Connect with us

Florent Ibenge ataja kikosi cha wachezaji 26

Florent Ibenge ataja kikosi cha wachezaji 26

Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Florent Ibenge Ikwange, amekitaja kikosi cha wachezaji 26 kujiandaa kumenyana na  timu ya Jamhuri ya Afrika ya Kati katika mchuano wa kufuzu katika fainali za mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2017 nchini Gabon.

Mchuano huo  utapigwa tarehe 6 mwezi Septemba jijini Bangui. Kikosi hicho kina makipa watatu, walinzi wanane, viungo wa kati saba na washambulizi wanane.

Ibenge amewaita pia wachezaji watatu wapyya wanaocheza soka nje ya nchi ambao ni pamoja na Paul-José Mpoku Chievo Verona (Italia), Remy Mulumba Lorient (Ufaransa) and Jirès Kembo Al Nasr (Dubai).

Shirikisho la soka FECOFA limetangaza kuwa mazoezi rasmi yataanza siku ya Jumatatu tarehe 31  jijini Kinsasha.

Kikosi kamili:  Makipa ( 3) 1. Kudimbana Nicaise (Antwerp- Ubelgiji)2. Kiassumbua Joel (Fc Wohlen – Usiwzi)3. Parfait Mandanda (Charleroi- Ubelgiji).

Mabeki  (8)  4. Oualembo Chistopher (Academica Coimbra – Ureno)5. Issama Mpeko Djo (TP Mazembe – DR Congo)6. N’sakala Fabrice (Anderlecht Ubelgiji)7. Chris Mavinga (FC Rubin Kazan – Urusi)8. Gabriel Zakuani (Peterborough – Uingereza)9. Kimwaki Mpela Joel (TP Mazembe – DR Congo)10. Cedric Mongongu (Eskisehirspor – Uturuki)11. Ungenda Bobo (Kabuscorp – Angola) .

Viungo wa kati (7)  12. Chancel Mbemba (New Castel United – Uingereza)13. Remy Mulumba (Lorient – Ufaransa) Cedrick Makiadi 14. (Bremen – Ujerumani)15. Kamavuaka Wilson (Sturm Graz – Austria)16. Paul-Jose Mpoku (Chievo Verona – Italia)17. Kebano Neeskens (Charleroi – Ubelgiji)18. Nkololo Jordan (Caen – Ufaransa)

Washambuliaji  (8)  19. Yannick Bolasie Yala (Crystal palace – Uingereza)20. Mubele Ndombe Firmin ( Al Ahli SC – Qatar )21. Jeremy Bokila (Guangzhou RF – China)22. Mabwati Cedric ( Columbus Crew SC – Marekani )23. Botaka Jordan ( Excelsior Rotterdam -Uholanzi )24. Kabananga Junior ( FC Astana – Kazakhstan)25. Cedric Bakambu (Bursaspor – Uturuki)26. Kembo Jirès ( Al Nasr – Dubai ).

CHAN 2020 MATCHES

Must See

More in