Connect with us

Frank Nuttal aichoka Gor Mahia

Frank Nuttal aichoka Gor Mahia

 

Kocha wa klabu ya soka ya Gor Mahia nchini Kenya Frank Nuttall ameondoka katika klabu hiyo na kujiunga na klabu ya Zamalek ya Misri kama kocha msaidizi.

Raia huyo wa Scotaland aliondoka jijini Nairobi Jumatatu asubuhi kwenda jijini Cairo kukamilisha mkataba wake na waajiri wake wapya.

Hatua hii inakuja baada ya kupoteza mchuano wake muhimu dhidi ya watani wao jadi AFC Leopards kwa bao 1 kwa 0 mwishoni mwa juma lililopita katika uwanja wa Kimataifa wa Kasarani jijini Naiorbi.

Nuttal aliisaidia Gor Mahia kutetea taji lake mwaka uliopita baada ya kuchukua mikoba ya kocha wa zamani wa Harambee Stars Bobby Williamson aliyempendekeza kwa viongozi wa Gor Mahia.

Pamoja na hilo, duru zinasema mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil Jose Mercelo Ferrairra “Ze Maria anatarajiwa kuwasili jijini Nairobi wiki hii kuja kuzungumza na viongozi wa Gor Mahia .

Gor Mahia ambayo imepoteza mchuano mmoja msimu huu, ni ya 12 kwa alama tatu katika msururu wa ligi kuu baada ya kucheza michuano minne na mitatu kutoka sare.

Mchuano ujao utakuwa dhidi ya City Stars Jumamosi hii katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi.

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in