Connect with us

Gor Mahia kumenyana na RS Berkane mechi ya robo fainali

Klabu ya Gor Mahia kutoka nchini Kenya, imepangwa kucheza na RS Berkane ya Morocco katika mechi ya robo fainali, kuwania taji la Shirikisho barani Afrika.

Michuano hii inachezwa nyumbani na ugenini na Gor Mahia itaanza kwa kuwakaribisha wapinzani wao jijini Nairobi, tarehe saba mwezi Aprili, kabla ya kurudiana tarehe 14.

Kuelekea katika hatua hiii, RS Berkane, iliongoza kundi la A, kwa alama 11, na kati ya mechi sita ilizocheza, ilishinda tatu na kufungwa moja.

Gor Mahia nayo, ilimaliza ya pili katika kundi la D kwa alama 9, baada ya kushinda mechi tatu na kufungwa nyingine tatu.

Nkana ya Zambia, itachuana na CS Sfaxien ya Tunisia, Hassania Agador nayo itamenyana na Zamalek ya Misri, huku Etoile du Sahel ya Tunisia ikipangwa na Al-Hilal ya Sudan.

Katika upande wa kuwania taji la klabu bingwa, Simba Sports Club ya Tanzania itamenyana na mabingwa mara tano wa taji hili TP Mazembe ya DRC.

Mechi hii itachezwa mwishoni mwa wiki ya kwanza ya mwezi Aprili na Simba wataanza kucheza nyumbani kabla ya mechi ya marudiano katika uwanja wa Kamalondo mjini Kamalondo baada ya majuma mawili.

Horoya ya Guinea, nayo itaanza nyumbani dhudi ya Wydad Casablanca, huku Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini ikimenyana na Al-Ahly ya Misri.

Nayo CS Constantine ya Algeria, itakuwa na kibarua dhid ya Esperance de Tunis ya Tunisia.

Gor Mahia kumenyana na RS Berkane mechi ya robo fainali

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in