Connect with us

Gor Mahia wanyimwa bao halali michuano ya Shirikisho

Bao la kusawazisha la Klabu ya Gor Mahia kutoka nchini Kenya, lilikataliwa katika mechi muhimu ya hatua ya makundi kuwania taji l;a Shirikisho barani Afrika dhidi ya timu ya NA Hussein Dey Jumapili usiku.

Bao hilo lilifungwa na beki kutoka nchini Uganda Shafik Batambuze katika dakika 59 baada ya mkwaju wa kona, na iwapo lingekubaliwa, mambo yangekuwa 1-1, lakini hilo halikubaliwa na mwamuzi kutoka Mali Boubou Traore.

Hatua hiyo, iliwakasirisha wachezaji na mashabiki wa Gor Mahia waliokuwa nchini Algier kushuhudia mechi hiyo.

Mechi hiyo ilikamilika kwa mabingwa wa soka nchini Kenya kupoteza kwa bao 1-0 na kuifanya Na Hussein Dey kuongoza kundi la D kwa alama saba.

Gor Mahia ni ya pili katika kundi hilo kwa alama 6, ikifuatwa na Zamalek ambayo ina alama tano baada ya kuishinda Petro de Luanda ya Angola bao 1-0 .

Al Hilal ya Sudan nayo imeendelea kupata matokeo mazuri baada ya kuishinda ZESCO UNITED ya Zambia kwa mabao 3-1 na inaongoza kundi la C kwa alama 7, ikifuatwa na Asante Kotoko ya Ghana ambayo nayo ilipata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Nkana ya Zambia.

Etoile du Sahel ya Tunisia, nayo ikiwa ugenini iliishinda Enugu Rangers ya Nigeria mabao 2-0 huku Salitas ya Burkina Faso ikatoshana nguvu kwa kutofungana na CS Sfaxien.

Kundi A, RS Berkane ya Morocco inaendelea kuongoza kundi hilo kwa alama nane licha ya kutoka 0-0 dhidi ya ndugu zao Raja Casablanca lakini AS Otoho, ya Congo Brazville iliishinda Hassania Agadir ya Morocco bao 1-0.

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in