Connect with us

Gor Mahia yakabidhiwa kombe la ligi kuu

Gor Mahia yakabidhiwa kombe la ligi kuu

Klabu ya Gor Mahia imekabidhiwa rasmi taji la ubingwa wa ligi kuu yas soka nchini humo msimu huu wa mwaka 2015.

Hatua hii inakuja baada ya kukamilika rasmi kwa ligi kuu ya soka nchini humo siku ya Jumapili jioni baada ya michuano ya mwisho.

Gor Mahia imemaliza vizuri msimu huu kwa kupata ushindi wa mabao 2 kwa 0 dhidi ya Muhoroni Youth mchuano uliochezwa katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi.

Klabu hiyo ambayo inanyakua ubingwa huu mara tatu mfululizo mwaka 2013, 2014 na sasa mwaka 2015 haijafungwa hata mchuano mmoja katika michuano 30 iliyocheza.

Msimu huu, Gor Mahia wameshinda mechi 24 na kwenda sare michuano sita na kufunga mabao 60 na kumaliza ligi hiyo kwa alama 78.

Nafasi ya pili imechukuliwa na mabingwa wa zamani wanajeshi Ulinzi Stars kwa alama 58 huku nafasi ya tatu ikiwaendea Sofapaka FC kwa alama 47.

Watani wa jadi wa Gor Mahia, AFC Leopards nao wamemaliza katika nafasi ya saba kwa alama 41 huku wawakilishi wa eneo la Pwani Bandari FC wakimaliza katika nafasi ya nne kwa alama 46.

Vlabu vya KCB na Nakuru All Stars vimeshushwa daraja msimu huu.

 

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in