Connect with us

Infantino achaguliwa tena rais wa FIFA hadi 2023

Gianni Infantino amechaguliwa kuongoza Shirikisho la soka duniani FIFA, kwa muhula wa pili wa miaka minne, utakaokamilika mwaka 2023.

Hatua hii imekuja baada ya kukosekana kwa mpinzani wa Infantino, wakati wa mkutano mkuu wa FIFA unaoendelea jijini Paris nchini Ufaransa.

Infantino, mwenye umri wa miaka 49 raia wa Uswisi na Italia, alichaguliwa kuwa rais wa FIFA mwaka 2016 baada ya kuondoka kwa rais wa zamani Sepp Blatter.

Baada ya kupata nafasi hiyo, kiongozi huyo wa FIFA amesema kuwa, wakati wa miaka mitatu ambao amekuwa madarakani, taswira ya soka duniani imebadilika na kuwa na maendeleo makubwa.

Wazo la Infantino , kuongeza mataifa yanayoshiriki katika kombe la dunia kutoka mataifa 32 hadi 48, limeshindikana kuanzia mwaka 2022 nchini Qatar kwa sababu za kisiasa.

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in