Connect with us

East Africa

Kenya yailemea Tanzania 3-2 AFCON 2019

Kenya yailemea Tanzania 3-2 AFCON 2019

Timu ya taifa ya soka ya Kenya imepata ushindi wake wa kwanza, katika michuano ya kuwania taji la bara Afrika inayoendelea nchini Misri, baada ya kuifunga majirani zao Tanzania mabao 3-2.

Harambee Stars ilitoka nyuma na kupata ushindi huo muhimu, katika pambano la timu hizo za Afrika Mashariki ambalo lilizua hisia nyingi kuelekea katika mchuano huo.

Michael Olunga alikuwa nyota wa Kenya, baada kuifungia mabao mawili, baada ya Johanna Ommolo kuisawazishia nchi yake bao la pili.

Tanzania walianza vema kwa kupata bao la mapema kupitia Saimon Msuva, huku nahidha Mbwana Samatta akifunga bao la pili kabla ya kipindi cha mapumziko.

Mechi ya mwisho Kenya itacheza na Senegal, kutafuta ushindi au sare ili kufuzu katika hatua ya 16 bora huku Tanzania ambayo imepoteza mechi mbili, ikisalia kumaliza kazi na Algeria.

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in East Africa