Connect with us

KMC imevunja mkataba na kocha wake Jackson Mayanja

KMC imevunja mkataba na kocha wake Jackson Mayanja

Na Mwandishi wetu akiwa Dar Es Salaam,

Baada ya mwanzo mbaya wa msimu wa KMC kwa kupokea vichapo vinne ndani ya mechi zao nane za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara ambayo inaendelea kwa sasa.

Uongozi wa KMC ya Kinondoni jijini Dar es Salaam umefikia hatua ya kuvunja mkataba na kocha wake Jackson Mayanja raia wa Uganda kwa kutoridhishwa na mwenendo wa timu hiyo ambayo imeshinda mechi 2 na kutoka sare mechi 2 kati ya nane.

KMC ambayo ilimaliza nafasi ya nne msimu wa 2018/19 ukiwa msimu wake wa kwanza Ligi Kuu, kwa sasa ipo nafasi za tano za mwisho (16) katika msimamo wa VPL wakiwa na alama 8 sawa na Biashara United waliopo nafasi ya 17 na Mbeya City waliopo nafasi ya 18 ila wametofautiana magoli ya kushinda na kufungwa.

Must See

More in