Connect with us

Kocha Migne ataja kikosi cha wachezaji 30 kuelekea fainali ya AFCON

Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Kenya Sebastien Migne amekitaja kikosi cha wachezaji 30 ili kuanza maandalizi ya michuano ya kuwania ubingwa wa mataifa ya Afrika, michuano itakayofanyika nchini Misri kuanzia mwezi Juni.

Kikosi hicho kinatarajiwa kwenda nchini Ufaransa kuanza maandalizi ya michuano hiyo mikubwa barani Afrika.

Migne raia wa Ufaransa, amemwacha nje beki David ‘Cheche’ Ochieng na mshambuliaji wa Zesco United nchini Zambia, Jesse Were.

Christopher Mbamba, anayechezea klabu ya Oskarshamns AIK nchini Sweden, ameitwa kwa mara ya kwanza katika kikosi cha Harambee Stars.

Mshambuliaji Allan Wanga, ana kibarua cha kumridhisha kocha Migne kuwa katika kikosi cha mwisho cha wachezaji 23, pamoja na Michael Olunga, Masoud Juma na Ayub Timbe.

Harambee Stars ambayo imepangwa katika kundi moja na Algeria, Senegal na Tanzania, itakwenda kuanza maandalizi jijini Paris na kuondoka tarehe 18 kwenda nchini Misri, siku tano kabla ya michuano hiyo.

Kikosi cha awali:-

Makipa: Patrick Matasi (St. Georges, Ethiopia), Faruok Shikhalo (Bandari FC, Kenya), John Oyemba (Kariobangi Sharks, Kenya), Brian Bwire (Kariobangi Sharks).

Mabeki: Philemon Otieno (Gor Mahia-Kenya), Musa Mohammed (Nkana FC-Zambia), Joash Onyango (Gor Mahia-Kenya), Abud Omar (Sepsi Sfântu-Romania), David Owino (Zesco United-Zambia), Bernard Ochieng (Vihiga United-Kenya), Brian Mandela (Maritzburg United-Afrika Kusini), Erick Ouma (Vasalund IF-Sweden).

Viungo wa Kati: Victor Wanyama (Tottenham Hotspurs-England), Anthony Akumu (Zesco United-Zambia), Eric Johanna (IF Bromma-Sweden), Ismael Gonzales (UD Las Palmas-Spain), Francis Kahata (Gor Mahia-Kenya), Dennis Odhiambo (Sofapaka FC-Kenya), Johanna Omollo (Cercle Brugge-Belgium), Christopher Mbamba (Oskarshamns AIK-Sweden), Whyvonne Isuza (AFC Leopards, Kenya), Clifton Miheso (Ureno).

Washambuliaji: Paul Were (AFC Leopards-Kenya), Ayub Timbe (Beijing Renhe-China), Michael Olunga (Kashiwa Reysol-Japan), Allan Wanga (Kakamega Homeboyz-Kenya), John Avire (Sofapaka), Masud Juma (Libya), Ochieng Ovella (IF Vasalund, Sweden).

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in