Connect with us

Kocha wa Simba SC kakiri alikuwa London kufuatilia kazi Tottenham Hotspurs

Kocha wa Simba SC kakiri alikuwa London kufuatilia kazi Tottenham Hotspurs

Na Mwandishi wetu akiwa Dar Es Salaam,

Baada ya kutoonekana mazoezini kwa siku zisizopungua tatu huku kukosekana kwake kukizua taharuki kubwa na kuzidisha uvumi kuwa klabu ya Simba SC imemfuta kazi kocha huyo.

Kuelekea mchezo dhidi ya Ruvu Shooting Patrick Aussems alirejea Tanzania na kuendelea na majukumu yake kama kawaida, waandishi walipomuuliza alikuwa wapi kiasi cha kukosekana mazoezi, Aussems alisema alienda London kufanya mazungumzo na Tottenham Hotspurs ili amrithi Mauricio Pochettino lakini bahati haikuwa yake nafasi hiyo kapewa Mourinho, kauli hiyo kaitoa akiwa mazoezini kupitia Azam TV

“Bahati mbaya kumekuwa na mvua nyingi jana na leo sio rahisi kufanya mazoezi mazuri lakini tumefanya kwa muda wa saa moja, nilikuwa london kufanya mazungumzo na Tottenham lakini kwa bahati mbaya wamemchukua  Mourinho” alitoa kauli Aussems ambayo ilitafsiriwa kama utani

Aussems hadi sasa karejea Dar es Salaam na atakuwa sehemu ya benchi la ufundi la Simba SC lakini bado kuna uvumi kuwa siku zake ndani ya Simba SC zinahesabika.

Hadi sasa Aussems ameiongoza Simba SC kucheza jumla ya michezo 9 ya Ligi Kuu akiwa na Simba SC akishinda michezo 7, sare mchezo mmoja na amepoteza mchezo mmoja akiwa nafasi ya pili kwa kuwa na alama 22, Kagera Sugar akiongoza Ligi kwakuwa na alama 23 ila ameizidi Simba SC kwa michezo miwili wakiwa wao wamecheza michezo 11.

Must See

More in