Connect with us

Ligi kuu Tanzania bara kurindima wikendi hii

Ligi kuu Tanzania bara kurindima wikendi hii

Ligi kuu ya Tanzania bara inaendelea Jumamosi na Jumapili mwishoni mwa juma hili katika viwanja mbalimbali baada ya mapumziko ya kupisha michuano ya Kimataifa.

Mchuano wa kati ya mabingwa watetezi Yanga FC na Azam FC ndio unaotarajiwa kuleta msisimko mkubwa siku ya Jumamosi.

Mechi hiyo itapigwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam na mashabiki wa vlabu vyote viwili wanatamba kuwa tumu yao itaibuka na ushindi.

Yanga wanajivunia wingi wa mashabiki, huku Azam wakitambuliwa na utajiri wa fedha.

Hadi sasa mechi tano zimechezwa katika msimu huu mpya wa ligi na Yanga na Azam wanafukuzana kila timu ikiwa na alama 15, ikifuatwa na Simba ambayo ina alama 12.

Ratiba Kamili.

Jumamosi Oktoba 17 2015

Young Africans

vs

Azam FC

Majimaji

vs

African Sports

Mbeya City

vs

Simba SC

Ndanda FC

vs

Toto Africans

Stand United

vs

Tanzania Prisons

Coastal Union

vs

Mtibwa Sugar

Jumapili Oktoba 18 2015

Mgambo JKT

vs

Kagera Sugar

Mwadui FC

vs

JKT Ruvu

Jumatano Oktoba 21 2015

Young Africans

vs

Toto Africans

Stand United

vs

Majimaji

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in