Connect with us

Ligi kuu ya soka nchini Uganda yapamba moto

Ligi kuu ya soka nchini Uganda yapamba moto

Mabao 15 yalifungwa wakati wa michuano ya ligi kuu ya soka nchini Uganda siku ya Jumanne.

Lweza FC ilipoteza mchuano wake wa pili msimu huu baada ya kufungwa na Express FC mabao 2 kwa 1 huku URA ikipata ushindi wa mabao 3 kwa 1 dhidi ya Soana FC.

Matokeo mengine yalikuwa kama ifuatavyo:-

Bright Stars F.C 1-1 Simba S.C

BUL F.C  0-0 Vipers S.C

Police F.C 1-1 The Saints F.C

Maroons F.C 0-1 Sadolin Paints F.C

SC Victoria University 1-2 SC Villa

Kwa matokeo hayo, KCCA FC inaongoza msururu wa ligi kwa alama 7 baada ya kucheza michuano mitatu, wakifutwa na URA ambao wana alama 4 baada ya mechi mbili.

Mabingwa watetezi Vipers FC ambao walitoka sare ya kutofungana wanashika nafasi ya 4 kwa alama tatu.

Michuano ijayo Jumanne tarehe 15 Septemba 2015 :-

Police Vs Sadolin Paints –Uwanja wa  Kavumba

Jinja Municipal Hippos Vs The Saints – Kakindu Stadium, Jinja

KCCA F.C Vs Simba – Nakivubo Stadium, Kampala

Maroons Vs Soana – Prisons Stadium, Luzira

Bright Stars Vs Express – Matugga

Lweza Vs SC Villa – Mutesa II Stadium, Wankulukuku

SC VU Vs Vipers – Nelson Mandela National Stadium

CHAN 2020 MATCHES

Must See

More in