Connect with us

Maendeleo ya Soka Afrika Yalimwinua Blatter

Maendeleo ya Soka Afrika Yalimwinua Blatter

Na Victor Abuso

Marais wa vyama vya soka barani Afrika kwa asilimia 100 walimpigia kura Sepp Blatter kuendelea kuongoza Shirikisho la soka duniani FIFA kwa muhula wa tano.

Hatua hii inaashiria namna Afrika inavyopenda Blatter na inapenda utendajikazi wake anavyosaidia ukuaji wa soka katika mataifa mbalimbali.

Joseph Sepp Blatter alipata kura 133 na kumshinda mshindani wake wa pekee Mwanamfalme kutoka Jordan Ali bin al-Hussein aliyepata kura 73 na kujiondoa kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa kura hiyo.

Lakini je, ni kwanini Afrika ilimpigia kura Blatter kwa asilimia 100 ?

Amaju Pannick rais wa Shirikisho la soka nchini Nigeria alinukuliwa akisema Blatter ni kiongozi anayeipenda Afrika, ana shauku ya kuona maendeleo ya soka katika mataifa hayo.

“Blatter ni kiongozi ambaye analipenda soka la Afrika,tumeona kazi aliyofanya na hatuwezi kuamini anayetoa ahadi sasa hivi , tuaamini kile tulichokiona,” alisisitiza.

Vongozi mbalimbali wa vyama vya soka barani Afrika wamekuwa wakisema kuwa bila Blatter, hapengekuwa na usawa katika soka duniani.

FIFA ikiongozwa na Blatter imekuwa ikitoa Mabilioni ya Dolla za Marekani, kujenga Ofisi za Mashirikisho katika nchi mbalimbali na hili limeonekana, ukitembea jijijni Nairobi nchini Kenya kwa mfano, jijini Dar es salaam Tanzania, utashuhudia ujezni wa Ofisi mpya.

Sababu nyingine ya Afrika kumchagua Blatter ni kwa sababu chini ya uongozi wake, amekuwa katika mstari wa mbele kujenga viwanja vipya vya nyasi bandia.

Afrika pia inaona kuwa Blatter hana upendeleo hasa baada ya kombe la dunia kuandaliwa barani Afrika nchini Afrika Kusini mwaka 2010, wengi wanaamini kuwa hii ilikuwa ni kazi ya Blatter ambaye amekuwa akisema anataka kuona michuano hii ikisambaa kote duniani.

Pamoja na hayo, viongozi wa Afrika wamekuwa wakisema kuwa FIFA chini ya Blatter imesaidia kuinua soka la vijana na kutoa fedha kusaidia kutafuta vipaji.

Katika nchi mbalimbali barani Afrika kwa sasa kuna michuano ya kila mwaka ya COPA COCACOLA .

Kwa sababu hizi, Joseph Sepp Blatter ameendelea kuaminiwa na viongozi wa soka barani Afrika na hivyo ataendelea kuongoza kwa muhula wa tano licha ya changamoto za ufisadi zinazoikabili FIFA.

 

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in