Connect with us

Mashabiki wa Yanga na Simba warushiana maneno

Mashabiki wa Yanga na Simba warushiana maneno

Mashabiki wa vlabu vya soka Yanga FC na Simba FC wamenza kurushiana maneno ya kishabiki siku mbili kabla ya mchuano muhimu wa watani wa jadi katika ligi kuu ya Tanzania bara kesho Jumamosi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Kila upande unavutia upande wake ukiwa na matumaini ya kupata ushindi.

Shaban Abdala mkaazi wa Magomeni, shabiki wa Yanga au maarufu vijana wa Jangwani amesema,

Jumamosi hii hawatuwezi, tutawafunga tatu bila,” alisisitiza.

Ni kweli katika siku za hivi karibuni wamekuwa wakitufunga lakini ya kale yamepita, msema kweli atajulikana Jumamosi,”. Aliongeza.

Sabina Martha mkaazi wa Tabata na shabiki wa Simba aliamaarufu Wekudu wa Msimbazi yeye anasema, Jumamosi klabu yake itaendeleza ubabe dhidi ya Yanga.

Wajua tumezoea kuwashinda hawa watani wetu, wakati ule ilikuwa tano bila, wakati mwingine 3 bila na Jumamosi najua itakuwa tano bila,” alisisitiza.

Katika mitandao ya kijamii, hivi ndivyo ilivyoandikwa kuelekea mchuano huo, Angurumaaaapo Simba Mcheza nani..? ANGURUMA… ANGURUMA… NGURUMA..!

Nao mashabiki wa Yanga wamekuwa wakiandika yafuatayo, “Eeh mwenyez mungu tuongoze wanao ktk kaz ya miguu yetu tuanze”.

paschalmusomiKesho yanga tupeni raha. Tunakiu ya siku nyingi sana”

HajimbwamboSimba hawachezi mpira ila wanaroga tu ila safari hii uchawi wao utadunda”

Chujikabilayani mnyama anakufa mbili bila”

CHAN 2020 MATCHES

Must See

More in