Connect with us

Matukio makubwa mwezi Januari na Februari 2016

Matukio makubwa mwezi Januari na Februari 2016

Januari  2016

Makala ya nne ya mashindano ya kuwania ubingwa wa Afrika katika mchezo wa soka baina ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza soka nyumbani CHAN, yataanza kutimua vumbi tarehe 16 mwezi huu wa Januari hadi mwezi Februari tarehe 7.

Michuano hii itafanyika nchini Rwanda.

Mataifa 16 yatashiriki katika michuano hii ambayo hufanyika kila baada ya miaka miwili tangu mwaka 2009.

Michuano hiyo itachezwa katika viwanja vinne, uwanja wa Amahoro jijini Kigali ulio na uwezo wa kuwakaribisha mashabiki elfu 30.

Uwanja wa Nyamirambo ambao pia upo jijini Kigali, uwanja wa Butare na ule wa Gisenyi.

Mataifa yaliyofuzu ni pamoja na wenyeji Rwanda, Uganda, DRC, Ethiopia, Zambia, Zimbabwe, Angola, Gabon, Cameroon, Nigeria, Niger, Ivory Coast, Mali, Guinea, Tunisia na Morocco.

Februari 2016

Mkutano Mkuu wa Shirikisho la soka duniani FIFA usiokuwa wa kawaida utafanyika tarehe 26 mwezi ujao wa pili katika Makao makuu ya Shirikisho hilo jijini Zurich nchini Uswizi.

Ajenda kuu ya Mkutano huu itakuwa ni kumchagua rais mpya wa FIFA kuchukua nafasi ya Sepp Blatter ambaye amepigwa marufuku ya kushiriki katika maswala ya soka kwa muda wa miaka minane kutokana na ufisadi katika Shirikisho hilo.

Wagombea wanaowania nafasi hiyo ni pamoja na:-

  • Mwanamfalme wa Jordan Ali bin Hussein, Makamu wa rais wa FIFA.
  • Salman Bin Ibhrahim Al-Khalifa, rais wa Shirikisho la soka barani Asia.
  • Jerome Champagne aliyekuwa Mwanakamati katika Shirikisho la soka duniani FIFA
  • Tokyo Sexwale mfanyibiashara kutoka Afrika Kusini.
  • Gianni Infantino Katibu Mkuu wa Shirikisho la soka barani Ulaya.

Must See

More in