Connect with us

Mckinstry akitaja kikosi cha kupambana na Senegal

Mckinstry akitaja kikosi cha kupambana na Senegal

 

Mshambuliaji Jacques Tuyisenge na beki Abouba Sibomana wanaoichezea klabu ya soka ya Gor Mahia nchini Kenya wamejumuishwa katika kikosi cha wachezaji 29 kuanza mazoezi siku ya Jumapili jijini Kigali.

Mchuano huo utakuwa maandalizi ya mchuano wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya Senegal katika uwanja wa Amahoro mwishoni mwa juma lijalo.

Kocha Johnny Mckinstry amesema mchuano huo wa kirafiki ni muhimu kwa sababu atautumia kuwapima wachezaji wake.

Baada ya mchuano huo wa kirafiki, Rwanda itachuana na Msumbiji katika mchuano wa kufuzu wa mataifa bingwa barani Afrika mwaka ujao nchini Gabon.

Mchuano huo utapigwa mapema mwezi ujao.

KIKOSI KAMILI

Makipa:

Ndayishimiye Eric (Rayon Sports), Mazimpaka Andre (Mukura), Ndoli Jean Claude (APR), Nzarora Marcel (Police)

Mabeki:

Rusheshangoga Michel (APR), Omborenga Fitina (SC Kiyovu), Ndayishimiye Celestin (Mukura), Sibomana Abouba (Gor Mahia,Kenya), Imanishimwe Emmanuel (Rayon Sports), Nirisrike Salomon (STVV, Belgium), Bayisenge Emery (APR), Rwatubyaye Abdul (APR), Kayumba Soter (AS Kigali) and Manzi Thierry (Rayon Sports)

Voungo wa Kati:

Bizimana Djihad (APR), Nshimiyimana Imran (Police), Mugiraneza Jean Baptiste (Azam, Tanzania), Mukunzi Yannick (APR), Niyonzima Ali (Mukura), Habyarimana Innocent (Police), Sibomana Patrick (APR), Iranzi Jean Claude (APR), Hakizimana Muhadjiri (Mukura), Nshuti Dominique Savio (Rayon Sports), Habimana Yussufu (Mukura), Niyonzima Haruna (Young Africans)

Wshambuliaji:

Usengimana Danny (Police), Uzumakunda Elias (Le Mans, France), Tuyisenge Jacques (Gor Mahia, Kenya) and Sugira Ernest (AS Kigali).

Must See

More in