Connect with us

Michezo ya Afrika: Senegal na Burkina Faso kuchuana fainali

Michezo ya Afrika: Senegal na Burkina Faso kuchuana fainali

Fainali ya mchezo wa soka katika mashindano ya Afrika inayoendelea jijini Brazzavile nchini Congo inachezwa leo Ijumaa kati ya Senegal na Burkina Faso.

Vijana wa Burkina Faso walifuzu baada ya kuifunga Nigeria mabao 3 kwa 1 katika hatua ya nusu fainali ya kusisimua siku ya Jumanne jioni, huku Senegal nayo ikifuzu kwa kuishinda wenyeji Congo Brazzaville pia kwa mabao 3 kwa 1.

Mashindano haya ya soka yanawajumuisha wachezaji wasiozidi umri wa miaka 23.

Siku ya Alhamisi, Nigeria ilimaliza katika nafasi ya tatu baada ya kuwafunga wenyeji wa michezo hii Congo kwa mabao 5 kwa 3 baada ya mchuano huo kumalizika kwa sare ya kutofunga katika muda wa kawaida wa mchezo huo.

Kabla ya fainali hiyo, kutakuwa na mchuano wa fainali ya wanawake kati ya Ghana na Cameroon katika uwanja wa Kintele.

CHAN 2020 MATCHES

Must See

More in