Connect with us

Michuano ya ligi kuu nchini Uganda na Rwanda kuendelea leo

Michuano ya ligi kuu nchini Uganda na Rwanda kuendelea leo

Mechi nane za ligi kuu ya soka nchini Uganda zinechezwa leo Jumanne katika viwanja mbalimbali.

Vipers wanachuana na KCCA FC katika uwanja wa Buikwe, Soana FC watakuwa wenyeji wa SC Villa Club katika uwanja wa Kavumba huku Express FC wakimenyana na URA katika uwanja wa Wankulukuku jijini Kampala.

Mechi zingine za leo:

JMC Hippos Vs Police FC

The Saints FC Vs Bright Stars FC

Simba FC Vs Maroons FC

SC Villa Vs Bull FC

Sadolin Paints FC Vs Lweza FC

KCCA FC wanaongoza msururu wa ligi kwa alama 10, sawa na Vipers Sports Club huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Express FC na Police FC ambao wana alama tisa.

Ratiba kama hii inaendelea nchini Rwanda.

Police FC wanachuana na Bugeresa FC, Espoir dhidi ya Kiyovu Sports, mabingwa watetezi APR dhidi ya Mukura na Amagaju wanachuana na Muhanga FC.

Ligi kuu ya soka nchini Rwanda ilianza mwishoni mwa juma liilopita.

CHAN 2020 MATCHES

Must See

More in