Connect with us

Michuano ya Shirikisho kuanza Jumapili

Michuano ya hatua ya makundi, kuwania taji la Shirikisho barani Afrika itaanza kuchezwa siku ya Jumapili katika mataifa mbalimbali barani Afrika.

Klabu 16 zimepangwa katika makundi manne, kutafuta taji hili ambalo linashikiliwa na Raja Casablanca ya Morocco.

Kundi A, Hassania Agadir, RS Berkane, Raja Casablanca zote za Morocco na AS Otoho ya Congo Brazaville

Kundi B, Etoile du Sahel, CS Sfaxine kutoka Tunisia, Unugu Rangers ya Nigeria na Salitas ya Burkina Faso.

Kundi C, ZESCO United ya Zambia, Al-Hilal ya Sudan, Asante Kotoko ya Ghana na Nkana ya Zambia.

Kundi D, Gor Mahia ya Kenya, NA Hussein Dey ya Algeria, Petro de Luanda ya Angola na Zamalek ya Misri.

Ratiba ya Jumapili, Februari 3 2019:

Gor Mahia vs Zamalek

ZESCO United vs Nkana

Al Hilal vs Asante Kotoko

Etoile du Sahel vs CS Sfaxien

Enugu vs Salitas

Na Hussein Dey vs Petro de Luanda

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in