Connect with us

Na Fredrick Nwaka,

Dar es Salaam. Kocha mkuu wa Taifa Stars Salum Mayanga amewaongeza kweny kikosi chake viungo Jonas Mkude wa Simba na Mudathir Yahya wa Singida United katika kikosi kitakachocheza na Benin.

Tanzania itasafiri kwenda Benin kuchuana na timu ya Taifa ya nchi hiyo katika mchezo wa kurafiki utakaochezwa Novemba 12.

Wachezaji hao walioongezwa wanachukua nafasi ya Erasto Nyon na Mzamiru Yasin ambao watakosa mchezo huo kwa sababu ya kadi nyekundu walizopata katika mchezo wa kirafiki uliopita dhidi ya Malawi.

Wakati huohuo kikosi cha Taifa Stars kitaingia kambini Novemba 5 kujianda na mchezo.

Ofisa Habari wa TFF, Alfrec Luas amesema mchezo huo ni muhimu na mwalimu ana matarajio makubwa na mchezo huo.

“Hii ni mechi muhimu na mwalimu ameipa kipaumbele kikubwa, timu itaingia kambink mapema kujiandaa,”amesema Lucas

More in East Africa