Connect with us

Msimu wa ligi kuu nchini Somalia kuanza Jumatatu

Msimu wa ligi kuu nchini Somalia kuanza Jumatatu

Shirikisho la soka nchini Somalia SFF limetoa ratiba ya ligi kuu ya soka nchini humo mwaka 2016.

Ligi hiyo itaanza kupigwa siku ya Jumatatu juma lijalo na kutakuwa na vlabu 10 vitakavyoshiriki.

Dekedda FC itafungua ligi hiyo kwa mchuano kati ya Heegan FC hawa ni maafisa wa polisi ambao ni mabingwa watetezi wa ligi hiyo.

Kuwepo kwa wachezaji wa kulipwa kutoka nchi nyingine kumeifanya ligi kuu kuwa na ushindi mkubwa katika siku za hivi karibuni.

Msemaji wa SFF Shafi’i Mohyaddin Abokar amesema, “ Zaidi ya asilimia 95 ya raia wa Somalia wanapenda sana soka na tumeamua kuwa michuano itakuwa inachezwa kutoka siku ya Jumatatu hadi Ijumaa,”.

Viongozi wa soka nchini humo wanasema wanatarajiwa kuwa msimu huu mpya kutakuwa na ushindani mkubwa msimu huu.

Kuimarika kwa usalama nchini Somalia kumeleta matumaini ya kuendelea kwa soka nchini humo.

Wiki moja iliyopita kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu, Shirika la taifa la Utangazaji SNTV lilionesha mchuano wa kuwania taji la Jenerali Da’ud.

Must See

More in