Connect with us

Na Fredrick Nwaka,

Dar es Salaam. Timu ya Mtibwa Sugar, Ndanda na Mbeya City zimevuna ushindi kwenye michuano ya ligi kuu iliyokamilika jioni hii nchini Tanzania.

Mtibwa imeitandika Prisons bao 1-0, Ndanda imeicharaza Lipuli bao 1-0 na Mbeya City imeichapa Ruvu Shooting mabao 2-0.

Azam imebanwa mbavu na Mbao fc kwa kulazimishwa sare ya bila kufungana mchezo uliochezwaa Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Michezo hiyo ni ya mzunguko wa saba na ile ya mzunguko wa nane itachezwa wiki ijayo ukiwemo mpambano mkali wa watani wa jadi Simba na Yanga.

More in