Connect with us

Mwenyekiti wa Gor Mahia ajitosa kuwania urais wa FKF

Mwenyekiti wa Gor Mahia ajitosa kuwania urais wa FKF

Mwenyekiti wa klabu ya soka ya Gor Mahia nchini Kenya, Ambrose Rachier ametangaza kuwania urais wa Shirikisho la soka nchini humo FKF.

Rachier ambaye ni Wakili amesema baada ya mashauriano ya muda mrefu amefikia uamuzi wa kuwania wadhifa huo kwa lengo la kuinua mchezo wa soka katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Licha ya kuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Gor Mahia, Rachier pia ni Mwenyekiti wa ligi kuu nchini humo KPL wadhifa alioupata baada ya klabu yake kuibuka mabingwa miaka mitatu iliyopita lakini pia ndio mabingwa wa mwaka huu.

Chini ya uongozi wa Rachier, Gor Mahia imekuwa ikifanikiwa katika michuano ya ligi kuu nchini humo kwa misimu mitatu sasa na anasema uzoefu wake utamsaidia kulete mabadiliko katika mchezo huo.

Wagombea wengine ni pamoja na rais wa sasa Sam Nyamweya, aliyekuwa Makamu wake Sam Shollei na Mwenyekiti wa klabu ya Kariobangi Sharks Nick Mwenda.

Uchaguzi huo utafanyika tarehe 13 mwezi Novemba ukitanguliwa na ule wa Matawi mbalimbali tarehe 29 mwezi Oktoba.

CHAN 2020 MATCHES

Must See

More in