Connect with us

Nigeria na Ghana kumenyana katika michuano ya Afrika

Nigeria na Ghana kumenyana katika michuano ya Afrika

Michuano ya hatua ya makundi kuwania taji la Afrika katika mashindano ya All Africa Games inaendelea siku ya Jumatano jijini Brazaville nchini Congo.

Wachezaji wanaoshiriki katika mashindano haya ni wale wenye umri usiozidi miaka 23.

Nigeria inachuana na Ghana katika mchuano wa kundi la B huku Burkina Faso ikimenyana na wenyeji Congo Brazaville siku ya Alhamisi.

Mchuano mwingine utakuwa ni kati ya Sudan na Zimbabwe.

Kundi la kwanza linaongozwa na Congo Brazaville kwa alama 3 sawa na Burkina Faso ambayo ni ya pili. Sudan na Zimbabwe hawana alama katika kundi hilo.

Nalo kundi la pili linaoongozwa na Senegal na Ghana ambao wana alama 1 huku Misri na Nigeria wakiwa hawana alama baada ya mchuano wao wa ufunguzi.

Misri ilijiondoa katika mashindano haya baada ya kutoa taarifa za dakika za lala salama kuwa kikosi chake kilikuwa dhaifu .

Michuano ya nusu fainali itachezwa tarehe 15 na mshindi wa kwanza na mshindi wa kundi la pili watakutana na katika mchuano wa kwanza wa nusu fainali huku mshindi wa kundi la pili wakicheza na mshindi wa kundi la kwanza.

Fainali itachezwa tarehe 18 mwezi huu.

 

CHAN 2020 MATCHES

Must See

More in