Connect with us

Nyamweya achunguzwa kwa madai ya ufujaji wa fedha

Nyamweya achunguzwa kwa madai ya ufujaji wa fedha

Rais wa Shirikisho la soka nchini Kenya FKF Sam Nyamweya na maafisa wengine wawili wanachunguzwa kwa tuhma za matumizi mabaya ya fedha.

Ofisi ya kiongozi wa mashtaka ya umma jijini Nairobi, inasema inachungunza namna Dola 170,000 zilizotengwa na serikali kuisaidia timu ya taifa Harambee Stars kwenda nchini Cape Verde zilivyotumiwa.

Wengine wanaochunguzwa ni pamoja na Katibu wa Shirikisho hilo Michael Esakwa na Samson Cherop Kaimu Meneja wa maswala fedha.

Harambee Stars ilichelewa kwenda nchini Cape Verde wakati wa mchuano wao wa kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi mwezi Novemba baada ya ndege waliyokuwa wamekodiwa na serikali kushindwa kuondoka jijini Nairobi kwa ukosefu wa nauli.

Hata hivyo,viongozi hao wa soka wanakanusha kuhusika kwa vyovyote vile na kupotea kwa fedha za serikali.

Yote haya yanafanyika wakati huu uchaguzi wa viongozi wapya wa soka ukitarajiwa kufanyika nchini humo kwa muda wa miezi kadhaa ijayo, na Sam Nyamweya ni miongoni mwa wagombea wa wadhifa huo.

Must See

More in