Connect with us

Rayon Sport na APR waanza vema ligi kuu nchini Rwanda

Rayon Sport na APR waanza vema ligi kuu nchini Rwanda

Mabingwa wa mwaka 2013 wa ligi kuu ya soka nchini Rwanda Rayon Sport wameanza vema msimu mpya wa ligi kuu nchini humo kwa ushindi wa mabao 2 kwa 0 katika mchuano wake wa ufunguzi uliopigwa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Marines FC.

Rayon Sport walipata magoli yote mawili kupitia wachezaji wake Imanshimwe Djaber na Kasirye Davis katika kipindi cha pili cha mchezo huo katika mchuano uliopigwa katika uwanja wa Rubavu.

Mbali na mchuano huo, klabu iliyopandishwa daraja ya Rwamagana City FC ilitoka sare ya kutofungana na AS Kigali katika uwanja wa Mumena.

Ligi hiyo inayofadhiliwa na Kampuni ya Tanzania ya Azam ilifungua milango yake siku ya Ijumaa iliyopita kwa mchuano wa kati ya mabingwa watetezi wa taji la Amani Police FC ambao waliwashinda Mukura mabao 2 kwa 1 katika uwanja wa Muhanga, huku Bugesera FC ambao pia wamepandishwa daraja msimu huu wakilazimisha sare ya kutofungana na Sports Club Kiyovu mechi iliyopigwa katika uwanja wa Nyamata.

Mabingwa watetezi APR, nao walianza vizuri kwa ushindi wa bao 1 kwa 0 dhidi ya Etincelles katika uwanja wa Tam Tam wilayani Rubavu.

Michuano hiyo inaendelea siku ya Jumanne na Jumatano juma hili.

Ratiba ya siku ya Jumanne Septemba 21 2015.
Police FC vs Bugesera FC (Uwanja wa Kicukiro)
Espoir FC vs SC Kiyovu (Uwanja wa Rusizi)
APR FC vs Mukura V.S (Uwanja wa Mumena)
Amagaju FC vs AS Muhanga (Uwanja wa Nyamagabe)

Siku ya Jumatano Septemba 22 2015

Rwamagana City FC vs Etincelles FC (Uwanja wa Rwamagana )

Musanze FC vs Gicumbi FC (Uwanja wa Musanze)

Rayon Sports FC vs AS Kigali (Uwanja wa Muhanga)

Marines vs Sunrise FC (Uwanja wa Tam Tam)

CHAN 2020 MATCHES

Must See

More in