Connect with us

Rwanda inaweza kuishinda Ghana Jumamosi ?

Rwanda inaweza kuishinda Ghana Jumamosi ?

Timu ya taifa ya soka ya Rwanda, Amavubi Stars inajiandaa kumenyana na Ghana siku ya Jumamosi katika mchuano muhimu kutafuta nafasi ya kucheza katika fainali za mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2017 nchini Gabon.

Amavubi Stars watakuwa nyumbani katika uwanja wa Amahoro kuwakabili Black Stars katika mchuano ambao umeanza kuzua hisia kwa mashabiki wa Rwanda na Ghana.

Kuna wale wanaosema kuwa mchuano huo utakuwa kama vita vya Daudi na Goliath huku wengine wakiona kuwa Rwanda ina nafasi nzuri ya kutumia uwanja wa nyumbani na kupata ushindi.

Mashabiki wa Ghana na baadhi ya wachambuzi wao wanaona kuwa historia ya Ghana katika soka la Afrika inaweza kuwasaidia katika mchuano huo wa Jumamosi na safari yao ya kuelekea Gabon.

Tangu mwaka 2004, Ghana wamekuwa wakifuzu katika mashindano ya mataifa bingwa barani Afrika na mwaka 2015 wakati michuano hii ilipofanyika nchini Equitorial Guinea, Black Stars ilifika katika hatua ya fainali.

Ghana pia inajivunia wachezaji wengi wanaocheza soka barani Ulaya.

Kikosi kamili:

Makipa : Razak Braimah (Cordoba, Uhispania), Fatau Dauda (AshGold), Richard Ofori (Wa All Stars)

Mabeki: Harrison Afful (Columbus Crew, Marekani), John Boye (Sivasspor, Uturuki), Jonathan Mensah (Evian, Ufaransa), Jeffery Schlupp (Leicester City, Uingereza), Baba Rahman (Chelsea, Uingereza), Gyimah Edwin (Orlando Pirates, Afrika Kusini), Daniel Amartey, (FC Copenhagen, Denmark)

Viungo vya Kati: Rabiu Mohammed (Krasnodar, Urusi), Emmanuel Agyemang-Badu (Udinese, Italia), Afriyie Acquah (Torino, Italia), Solomon Asante (T.P. Mazembe, DR Congo), Christian Atsu (Bournemouth, Uingereza), Andre Ayew (Swansea City, Uingereza) Mubarak Wakaso (Rubin Kazan, Urusi), Bernard Mensah (Getafe, Uhispania), Godfred Donsah (Bologna, Italia)

Washambualiji: Asamoah Gyan (SIPG Shanghai, China), Jordan Ayew (Aston Villa, Uingereza), Ebenezer Assifuah (Sion, Switzerland), David Accam (Chicago Fire, Marekani), Richmond Boakye Yiadom(Atalanta, Italia).

Rwanda nayo itakuwa inajivunia nahodha wake , Haruna Niyonzima ambaye anachezea klabu ya Yanga ya Tanzania.

Wengine ni pamoja na Emery Bayisenge, Salomon Nirisarike, Abouba Sibomana na kipa Olivier Kwizera.

Kikosi Kamili :

Makipa: Olivier Kwizera (APR), Jean Claude Ndoli (APR), Eric Ndayishimiye (Rayon), Michel Rusheshangoga (APR).

Mabeki: Fitina Omborenga (Kiyovu), Jean Marie Rukundo (Rayon Sports), Abouba Sibomana (Gor Mahia), Celestin Ndayishimiye (Mukura), Salomon Nirisarike (Saint Truiden), Emery Bayisenge (Lask Linz), Faustin Usengimana (APR), Ismael Nshutiyamagara (APR).

Viungo wa Kati: Jean Baptiste Mugiraneza (Azam), Djihad Bizimana (APR), Yannick Mukunzi (APR), Imran Nshimiyimana (Police), Haruna Niyonzima (Young Africans).

Washambuliaji: Andrew Buteera (APR), Jacques Tuyisenge (Police), Jean Claude Iranzi (APR), Patrick Sibomana (APR), Quentin Rushenguziminega (Lausanne Sport), Isaie Songa (Police), Ernest Sugira (AS Kigali), Michel Ndahinduka (APR).

Ghana na Rwanda zilipata ushindi katika michuano yao ya ufunguzi wa kundi lao na kujipatia alama tatu muhimu.

Rwanda ikiwa ugenini ilipata ushindi wa bao 1 kwa 0 dhidi ya Msumbiji jijini Maputo.

Ghana nao walianza vizuri kwa kupata ushindi wa mabao 7 kwa 0 dhidi ya Mauritius.

CHAN 2020 MATCHES

Must See

More in