Connect with us

Rwanda ilitoka nyuma na kulazimisha sare ya mabo 2-2 dhidi ya Uganda katika michuano ya soka baina ya wanawake katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati CECAFA, inayoendelea jijini Kigali.

Crested Cranes ya Uganda ilianza kwa kupata bao la mapema katika dakika ya 10 ya mchuano huo, kupitia Mutuuzo Lilian lakini Ibangarye Anne Marie’ aliisawazishia Rwanda kupitia mkwaju wa penalti.

Hata hivyo katika dakika ya 74, mchezaji wa Uganda Alupo Norah aliipa timu yake bao la pili, lakini katika Mukeshimana Jeanette akaizawazishia Rwanda katika dakika za nyongeza za mchuano huo.

Siku ya Alhamisi ni siku ya mapumziko kuelelea michuano ya mwisho siku ya Ijumaa, ambapo Rwanda itacheza na Kenya huku Tanzania ikimenyana na Ethiopia.

Matokeo rasmi

Alhamisi, Julai 19

Kenya 0-1 Uganda

Rwanda 1-0 Tanzania Mainland

Jumamosi, Julai 21

Ethiopia 1-2 Uganda

Kenya 1-1 Tanzania

Jumatatu Julai 23

Uganda 1-4 Tanzania

Rwanda 0-3 Ethiopia

Jumatano, Julai 25

Kenya 0-1 Ethiopia

Uganda 2-2 Rwanda

Ijumaa, Julai 27

Ethiopia v Tanzania – (Stade de Kigali, 8:00)

Rwanda v Kenya – (Stade de Kigali, 10:30)

Timu            M        U       K        D        W      K     TB     Alama

Uganda        4        2        1        1        6        7        -1       7

Ethiopia       3        2        1        0        5        3        2        6

Tanzania      3        1        1        1        5        2        3        4

Rwanda       3        1        1        1        4        5        -1       4

Kenya          3        0        2        1        1        3        -2       1

 

More in CECAFA Women's Senior Challenge