Connect with us

 

Shirikisho la soka nchini Rwanda FERWAFA, limetangaza orodha ya makocha 52 wote raia wa kigeni walioomba kazi ya kuifunza timu ya taifa Amavubi Stars.

Mwezi uliopita, FERWAFA ilitangaza kuwa ilikuwa inamtafuta kocha kujaza nafasi ya Jonathan McKinstry ambaye alifutwa kazi baada ya matokeo mabaya mwaka uliopita.

Kocha mpya anatarajiwa kuindaa Rwanda kufuzu katika michuano ya CHAN mwaka 2018 nchini Kenya, lakini pia kufuzu katika michuano ya mataifa ya Afrika nchini Cameroon mwaka 2019.

Miongoni mwa makocha walioomba kazi hiyo ni pamoja na aliyekuwa kocha wa Algeria George Leekens na aliyekuwa kocha wa Kenya Antoine Hey.

Wengine ni pamoja na Winfried Schafer, Samson Siasia, Dragomir Okuka, Tom Saintfiet, Peter Butler, Nikola Kavazovic, Sebastien Desabre, Goran Kopunovic, Didier Gomes da Rosa ,Engin Firat miongoni mwa wengine.

More in