Connect with us

Simba na Azam FC waanza vizuri ligi kuu Tanzania bara

Simba na Azam FC waanza vizuri ligi kuu Tanzania bara

Mabingwa wa zamani wa ligi kuu ya soka Tanzania bara, wameanza vema msimu mpya baada ya kupata ushindi mwembamba wa bao 1 kwa 0 katika mchuano wake wa kwanza dhidi ya African Sport.

Nao, matajiri wa jiji la Dar es salaam walianza kwa mkuu wa kulia kwa ushindi wa mabao 2 kwa 1 dhidi ya Tanzania Prisons wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani wa Chamazi.

Ndanda FC ikiwa nyumbani mjini Mtwara imetoka sare ya bao 1 kwa 1 na Mgambo JKT, huku Maji-Maji ya Songea ikiwashinda maafande wa JKT Ruvu bao 1 kwa 0.

Matokeo mengine, Mtibwa Sugar wakiwa ugenini wameilaza Stand United bao 1 kwa 0, Toto Africans nao wakiwashinda Mwadui FC bao 1 kwa 0.

Wakata miwa Kagera Sugar nao walifurahia ushindi wa bao 1 kwa 0 dhidi ya Mbeya FC ugenini.

Siku ya Jumapili ni zamu ya mabingwa watetezi Yanga FC dhidi ya Coastal Union ya Tanzania katika mchuano utakaochezwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

CHAN 2020 MATCHES

Must See

More in