Connect with us

Na Fadhili Omar Sizya,

Beki raia wa Burkina Faso Zana Coulibally (26) amekamilisha rasmi kusajiliwa na mabingwa watetezi ligi kuu ya kandanda Tanzania bara Simba Sc akitokea Asec Mimosas ya Ivory Coast.

Kabla ya kusaini kandarasi, beki huyo alifanyiwa vipimo vya afya ya moyo (ECHO Cardiogram)  chini ya daktari George Longopa kutoka taasisi ya moyo Jakaya Kikwete (JKCI).

Beki huyo anayecheza upande wa kulia amejiunga na wekundu hao wa msimbazi kuziba nafasi hiyo baada ya mlinzi Shomari Kapombe kupata majeraha na kukosekana uwanjani miezi miwili.

Ikumbukwe Simba inashiriki michuano ya klabu bingwa Afrika hivyo ujio wa beki huyo ni kuzidi kuimarisha kikosi hicho ambacho kimekuwa kikifanya usajili wa wachezaji wenye majina makubwa barani afrika.

Coulibally anahitimisha wachezaji watano kutoka ukanda wa magharibi, akiungana na Pascal Wawa(Ivory Coast), Nicolas Gyan,James Kotei na Asante Kwasi (Ghana).

 

More in