Connect with us

Simba SC yamtangaza Salim Kikeke wa BBC kama balozi wao

Simba SC yamtangaza Salim Kikeke wa BBC kama balozi wao

Na Mwandishi wetu akiwa Dar Es Salaam,

Klabu ya soka ya Simba SC ya Tanzania imeamua kumtangaza mwandishi wa habari na mtangazaji wa BBC Salim Kikeke kuwa ndiye balozi wa klabu hiyo jijini London nchini Uingereza, maamuzi hayo yamefikiwa baada ya bodi ya wakurugenzi kukaa na kupitisha kitu hicho kipya.

Kikeke ametangazwa kuwa balozi wa hiari na kutokana kuwa na mapenzi na mchezo wa mpira wa miguu hususani klabu ya Simba SC wamefikia maamuzi hayo, baada ya Kikeke kuwa shabiki mkubwa wa Simba SC kwa muda mrefu.

“Lengo letu hasa ni kukuza soka la Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla wake, hili ni jambo jipya kwa mimi kuweza kuwa balozi wa kwanza kabisa wa klabu hii, majukumu yake ya kimsingi kwa sasa ni kuangalia namna ya kukusanya mashabiki wa Simba hapa Uingereza na kuweza kukaa na kuangalia tunaipeleka wapi klabu ya Simba” alisema Salim Kikeke

Kwa mujibu wa Kikeke amenukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini Tanznaia akisema ubalozi wake wa hiari na wenye lengo wa kukuza na kutangaza soka la Afrika Mashariki ila jukumu lake kubwa katika jiji la London litakuwa ni kuitangaza vyema Simba SC

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in