Connect with us

Simba wapata ushindi mkubwa ligi kuu Tanzania bara

Simba wapata ushindi mkubwa ligi kuu Tanzania bara

Michuano ya ligi kuu ya soka Tanzania bara iliendelea mwishoni mwa juma huku michuano minne ikichezwa siku ya Jumapili katika viwanja mbalimbali.

Mabingwa wa zamani Simba FC kutoka mitaa ya Msimbazi jijini Dar es salaam wakiwa katika uwanja wa taifa ,walipata ushindi mkubwa wa mabao 3 kwa 1 dhidi ya Kagera Sugar kutoka Bukoba.

Mchezaji wa Kimataifa kutoka Uganda Hamis Kiiza aliipa timu yake mabao yote matatu na kuwa nyota wa mchezo huo, huku Mubarak Yusuf akiipa Kagera bao pekee la kufuta machozi.

Mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati Azam FC nao walipata wakati mgumu mbele ya Mwadui FC kwa kupata bao 1 kwa 0.

Bao la pekee la Azam lilitiwa kimyani na John Bocco.

Matokeo kamili mwishoni mwa juma:-

Jumapili Septemba 20 2015

Mwadui FC

0

1

Azam FC

16:00

Mtibwa Sugar

2

1

Ndanda FC

16:00

Simba SC

3

1

Kagera Sugar

16:00

Coastal Union

0

0

Toto Africans

16:00

Jumamosi Septemba 19 2015

Stand United

2

0

African Sports

16:00

Mgambo JKT

1

0

Majimaji

16:00

Tanzania Prisons

1

0

Mbeya City

16:00

Young Africans

4

1

JKT Ruvu

16:00

Msimamo kuu wa ligi kuu Tanzania

#

Timu

MEC

ALAMA

1 Young Africans 3 9
2 Simba SC 3 9
3 Azam FC 3 9
4 Mtibwa Sugar 3 9
5 Majimaji 3 6
6 Ndanda FC 3 4
7 Toto Africans 3 4
8 Mgambo JKT 3 4
9 Mbeya City 3 3
10 Mwadui FC 3 3
11 Stand United 3 3
12 Kagera Sugar 3 3
13 Tanzania Prisons 3 3
14 Coastal Union 3 1
15 African Sports 3 0
16 JKT Ruvu 3 0

CHAN 2020 MATCHES

Must See

More in