Connect with us

Sudan Kusini yapanda orodha ya FIFA

Sudan Kusini yapanda orodha ya FIFA

Timu ya taifa ya soka ya Sudan Kusini imepanda nafasi kumi na kufikia 134 kwa mujibu wa orodha mpya ya Shirikisho la soka duniani FIFA.

Tanzania ambayo ipo nchini Afrika Kusini inapojiandaa kwa mchuano muhimu wa kufuzu katika kombe la dunia mwaka 2018 imeshuka nafasi moja na sasa ni ya 135.

Uganda Cranes ambayo imeendelea kuwa timu bora katika ukanda wa CECAFA imeendelea kuongoza na ni ya 68 ikifuatwa na Rwanda ambayo ni ya 96 dunaini.

Burundi ni 107, Ethiopia 114 , Kenya 125 huku Sudan ikiwa ya 128 kwa mujibu ya orodha hiyo ya mwezi huu.

Timu bora barani Afrika ni Ivory Coast ikifuatwa na Algeria huku Ghana ikiwa ya tatu na ya 30 duniani.

Orodha nyingine duniani Cape Verde 32 ,Senegal 39

Tunisia 41 , Cameroon 51, Congo, Guinea 53 huku Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ikiwa ya 55.

Must See

More in