Connect with us

Tanzania: Mashabiki wa Simba na Yanga watakiwa kuepuka siasa uwanjani

Tanzania: Mashabiki wa Simba na Yanga watakiwa kuepuka siasa uwanjani

Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF linatoa wito kwa mashabiki wa klabu ya Yanga na Simba kutojihusisha na siasa wakati wa mchuano kati ya timu hizo mbili siku ya Jumamosi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Msemaji wa Shirikisho hilo Baraka Kizuguto akizungumza na wanahabari katika makao makuu ya TFF katika uwanja wa Karume jijini Dar es salaam, amesisitiza kuwa wao kama viongozi wa soka hawaegemei upande wowote wa kisiasa.

Kauli hii imekuja baada dhana kuwa mashabiki wa Yanga wanaengemea upande wa chama tawala CCM kwa sababu ya rangi ya jezi ya klabu hiyo ya kijani na njano ambazo ndizo cham cha rangi ya CCM.

Wakati wa mchuano wa Tanzania na Nigeria, mwanasiasa Januari Makamba wa chama cha CCM alijitolea kuwalipia kiingilio mashabiki kuingia uwanja na kuzua hisia za kisiasa kati ya mashabiki wa chama tawala na upinzani.

Tunawaomba mashabiki watakaokuja uwanjani wasiingize hisia za kisiasa katika mchezo wa Jumamosi lakini wahudhurie na kuondoka kwa amani,” alisisitiza Kizuguto.

Mbali na suala hilo la kisiasa, TFF inasema maandalizi ya mchuano huo wa Jumamosi umekamilika na tayari mashabiki wa Simba na Yanga wameshaanza kubishana kuhusu ni nani atakayeibuka mshindi.

Aidha, viingilio vya mchuano huo vimewekwa wazi kuelekea mchuano huo kati ya watani hao wa jadi.

Kiingilia cha juu zaidi kitakuwa ni Shilingi za Tanzania 30,000 20,000 na kile cha chini kitakuwa ni Shilingi 7,000 na tiketi hizo zitaanza kuuzwa kuanzia saa mbili asubuhi siku ya Jumamosi.

Refarii mkongwe Isreal Nkongo kutoka Dar es salaam amepewa jukumu la kuchezesha mchuano huo wa kihistoria.

CHAN 2020 MATCHES

Must See

More in