Connect with us

Tanzania Prisons bado inatafuta mbabe wake ligi kuu, Simba kamcheka

Tanzania Prisons bado inatafuta mbabe wake ligi kuu, Simba kamcheka

Na Mwandishi wetu akiwa Dar Es Salaam,

Mabingwa wa Ligi Kuu soka Tanzania bara Simba SC baada ya kucheza mechi 8, wakifungwa mechi 1 na ushindi mechi 7,  ndio walikuwa wanaaminika kuwa katika mchezo wake wa tisa  dhidi ya Tanzania Prisons ndio watavunja rekodi ya Prisons ya kutofungwa lakini mambo yamekuwa tofauti. 

Simba SC kwenye uwanja wake wa Uhuru ambao wanatumia kama uwanja wao wa nyumba, wamelazimishwa sare 0-0 na kugawana point moja moja..

Kwa sasa Tanzania Prisons inabakia kuwa timu pekee Ligi ya Tanzania bara ambao hawajawahi kupoteza mchezo hadi sasa wakiwa wamecheza mechi 10.

Simba  anaongoza Ligi kwa sasa kwa kuwa na point 22, walizopata katika michezo 9 waliocheza, akipoteza mchezo mmoja na sare 1, huku Prisons wakishika nafasi ya nne kwa kuwa na point 16, wakicheza michezo 10, sare 7 na ushindi mechi 3.

Must See

More in