Connect with us

Na Fredrick Nwaka,

Dar es Salaam. Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ wamesema licha ya ugumu wa mchezo wa kirafiki dhidi ya Malawi wamenuia kuibuka na ushindi.

Tanzania na Malawi ‘The Flames’ zitachuana kesho kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaochezwa Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Mshambuliaji Mbwana Samatta alisema kazi kubwa ni kuhakikisha wanapata ushindi.

“Mechi ni ngumu kw sababu Tanzania na Malawi tunafahamiana kwa muda mrefu, wao wana wachezaji wazuri lakini sisi pia tumejiandaa,’alisema Samatta.

Beki wa Baroka FC, Abdi Banda alsema hiyo ni mechi muhimu kwa kila mchezaji ili kuliletea sifa taifa.

Mecho hiyo itaanza saa kumi kamili kwa saa za Afrika Mashariki na itainyeshwa na kituo cha luninga cha Azam.

More in East Africa