Connect with us
2015 the year in numbers

Tovuti yetu mwaka 2015

Tovuti yetu mwaka 2015

Heri ya mwaka mpya wapenzi wasomaji wa tovuti yetu ya soka25east.com.

Mwaka 2015 ulikuwa wa mafanikio makubwa sana lakini hatukukosa changamoto mbalimbali.

Mwezi Februari mwaka uliopita, tuliadhimisha mwaka mmoja na kipindi hicho tulitaka kuwa na kasi mpya ili kupata wasomaji zaidi.

Tulikuwa na lengo la kukuletea wewe msomaji wetu habari za hivi punde kuhusu mchezo wa soka barani Afrika.

Changamoto.

Tuliweka mfumo ambao ungetusaidia tunapochapisha habari zetu za soka kutokuwa na msongamano mkubwa wa habari.

Hata hivyo, muda mfupi baada ya kuweka mfumo huo tulikumbana na changamoto ya msongamano huo.

Kati ya mwezi Juni na Julai, kulikuwa na msongamano mkubwa na ikawa vigumu sana kuchapisha taarifa nyingi za soka.

Hii ilitulazimu kubadilisha mtandao unaotusaidia kuchapisha taarifa zetu, hatua ambayo iliwasaidia wasomaji wetu kupata taarifa zetu wakitafuta soka25east.com au soka25east.

Waandishi wapya

Mwaka 2015, tovuti iliongeza waandishi wake kupanua wigo wake. Miongoni mwa wale waliojiunga ni pamoja na kikosi cha soka25east.com ni pamoja na Bonface OsanoAustin OduorAaron Mubanga JrKelvin Tradeu MusakoJames “Guru” SibelekiBwezani Mbewe, Evans Oduor, Vicent Kakooza, Lorraine Rutto, na mwanahabari wetu wa Kiswahili ,Victor “Kaka” Abuso.

Kwa ongezeko hili, tumeweza kukuleta taarifa za kina kutoka Afrika Mashariki, Kati, Kusini mwa Afrika pamoja na eneo la Kaskazini.

Tunakuletea pia taarifa za timu za taifa za soka kutoka bara lote la Afrika.

Heri ya mwaka mpya wa 2016.

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in