Connect with us

TP Mazembe yafungwa mchuano wa kutafuta nafasi ya tano

TP Mazembe yafungwa mchuano wa kutafuta nafasi ya tano

Klabu ya soka ya TP Mazembe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imefungwa mabao 2 kwa 1 na Club America kutoka Mexico kuibuka katika nafasi ya tano katika mashindano ya dunia baina ya vlabu nchini Japan.

Mabao ya Club America yalitiwa kimyani na Dario Benedetto na mwezake Martin Zuniga katika kipindi cha kwanza cha mchuano huo.

Bao la Benedetto lilitikisa nyavu za TP Mazembe katika dakika 19 ya mchuano huo huku Zuniga akifunga la pili katika dakika ya 29 huku Mazembe ikipata bao lake kupitia Rainford Kalaba katika dakika ya 43 ya kipindi hicho cha kwanza.

Baadhi ya mashabiki wanahisi kuwa maanadalizi ya TP Mazembe hayakuwa mazuri kuelekea michuano hiyo huku wengine wakidokeza kuwa ilikuwa ni tu bahati mbaya kwa timu yao kufungwa.

Michuano ya nusu fainali ni siku ya Alhamisi, Barcelona watachuana na Guangzhou Evergrande ya China huku Sanfrecce Hiroshima  ya  Japan ikichuana River Plate kutoka Argetina.

Watakaoibuka washindi watamenyana katika fanali siku ya Jumapili.

 

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in