Connect with us

Wachezaji 30 kuwania tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara itakayotolewa Juni 23 katika Ukumbi wa Mlimani City uliopo Jijini dare s salaam na wadhamini wa Ligi hiyo kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.

Klabu za Yanga, Simba na Azam ndizo zinaonekana kuwa na wachezaji wengi katika tuzo hizo.

Wachezaji 30 wanaowania tuzo ni Habibu Kyombo (Mbao), Khamis Mcha (RuvuShooting), Yahya Zayd, Razack Abalora, Bruce  Kangwa, Aggrey Morris , HimidMao –Azam, Awesu Awesu –Mwadui, Adam Salamba-Lipuli, Mohammed Rashid-Prisons, Shafiq Batambuze-Singida, Mudathir Yahya-Singida

Wengine katika orodha hiyo ni United, Marcel Kaheza- Majimaji, Ditram Nchimbi-Njombe Mji, Eliud Ambokile- Mbeya City,  Shaaban Nditi-Mtibwa, Tafadzwa Kutinyu-Singida, Ibrahim Ajibu, Gadiel Michael, Papy Tshishimbi, Kelvin Yondani, Obrey Chirwa-Yanga, Aishi Manula-Simba, Emmanuel Okwi, John Bocco, Jonas Mkude, Erasto Nyoni, Shiza Kichuya, Asante Kwasi –Simba na Hassan Dilunga-Mtibwa.

Tuzo nyingine zitakazotolewa ni Bingwa, Mshindi wa Pili, Mshindi wa Tatu, Mshindi wa Nne, Mfungaji Bora, Timu yenye nidhamu,U20 Player (Tuzo ya Ismail Khalfan),Mchezaji Bora Chipukizi

Mwamuzi Bora Msaidizi, Mwamuzi Bora, Kipa Bora, Kocha Bora, Goli Bora , VPL Best Eleven, Mchezaji wa heshima.

Zawadi kwa kila kategori pamoja na majina ya wanaowania tuzo ukiacha bingwa, mshindi wa pili, wa tatu, wa nne na mfungaji bora ambao hujulikana kulingana na ligi inavyoendelea zitatangazwa siku za usoni.

African journalist with passion of football reporting.Also i love politics

More in East Africa