Connect with us

Twiga Stars waangukia pua nyumbani

Twiga Stars waangukia pua nyumbani

 

Timu ya taifa ya soka ya wanawake ya Zimbabwe The Mighty Warriors, imeishinda Twiga Stars ya Tanzania mabao 2 kwa 1 katika mchuano muhimu wa kufuzu katika fainali ya mataifa bingwa barani Afrika, itakayochezwa mwezi Novemba mwaka huu nchini Cameroon.

Warembo wa Twiga Stars ilishindwa kutumia uwanja wao wa nyumbani wa Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es salaam Ijumaa jioni, licha ya kuanza kupata bao katika kipindi cha kwanza cha mchuano huo.

Mchuano wa marudiano utapigwa baada ya majuma mawili jijini Harare.

Zimbabwe imefuzu katika michuano ya Afrika mara tatu mwaka 2000, 2002 na 2004.

Tanzania imekuwa ikilemewa na Zimbabwe kwa muda mrefu na mwaka 2004, timu hizi mbili zilikutana katika mchuano wa robo fainali mwaka 2004 na Zimbabwe kupata ushindi.

Mshindi baada ya mechi ya mzunguko wa pili, atachuana na Zambia au Namibia katika hatua ya mwisho ya kufuzu katika fainali hiyo.

Mataifa mengine yanayotafauta nafasi hiyo ni pamoja na mabingwa watetezi Nigeria, Ghana,Equaitorial Guinea, Afrika Kusini na Ivory Coast.

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in