Connect with us

Urusi 2018: Algeria kuwasili nchini Tanzania Alhamisi

Urusi 2018: Algeria kuwasili nchini Tanzania Alhamisi

Timu ya taifa ya soka ya Algeria (The Desert Warriors) inatarajiwa kuwasili nchini Tanzania siku ya Alhamis kwa ndege binafsi ya kukodi, tayari kumenyana na wenyeji wao Taifa Stars katika mchuano wa kufuzu kucheza kombe la dunia utakaopigwa siku ya Jumamosi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Tayari kocha wa timu hiyo Christian Gourcuff raia wa Ufaransa amekitaja kikosi cha wachezaji 24, akiwemo wachezaji 18 wanaocheza katika klabu za Ulaya kwa ajili ya kuikabili Tanzania.

Kikosi kamili cha Algeria:-

Makipa: Doukha Izeddine (JS Kabliye), M’bolhi Rais (Antalyaspor), Asselah Malik (CR Belouizdad).

Mabeki : Zeffane Mehdi (Rennes), Medjani Carl (Trabzonspor), Ziti Mohamed (JS Kabliye), Mesbah Eddine (Sampordia), Bensebaini Ramy (Montpeller), Belkarou Hichem (Club African), Ghoulam Faouzi (Namples), Mandi Aissa (Reims).

Viungo wa kati: Guedioura Adlane (Watford), Boudebouz Ryad (Montpeller), Taider Saphir (Bologna), Abeid Mehdi (Panathinacos), Bentaleb Nabil (Tottenham), Ghezzal Rachid (Lyon), Melsoub Walid (Lorient), Marhez Ryad (Leicester).

Washambuliaji: Benrhama Said (Nice), Sliman Islam (Sporting Lisbon), Belfodil Ishak (Beni Yas), Brahimi Yassine (FC Porto) na Bounedjah Baghdad (Etoile du Saleh)

Tayari Shirikisho la soka nchini Tanzania TF limentangaza viingilio vya mchezo huo na bei ya chini itakuwa ni Shilingi 5,000 huku ile ya juu ikiwa ni Shilingi 10,000.

Kikosi cha timu ya Taifa Stars kinatarajiwa kurejea nyumbani kesho Jumatano mchana tayari kwa maandalizi ya mwisho ya mchezo huo.

Stars iliyoweka kambi nchini Afrika Kusini imekua ikifanya mazoezi kila siku katika uwanja wa Edenvale, ambapo mpaka sasa wachezaji wote wapo katika hali nzuri hakuna majeruhi na kila mmoja yupo tayari kwa mchezo wa Jumamosi.

Wachezaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaochezea klabu ya TP Mazembe Mazembe wanatarajiwa kuungana na wenzao kambini kesho jijini Dar ess alaam.

Mchuano huu utachezwa nyumbani na ugenini na mshidi atafuzu katika hatua ya makundi kuendelea kutafuta tiketi ya kufuzu kwenda Urusi.

 

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in