Connect with us

Urusi 2018:Micho akitaja kikosi kitakachovaana na Togo

Urusi 2018:Micho akitaja kikosi kitakachovaana na Togo

Kocha wa timu ya taifa ya soka ya Uganda Milutin ‘Micho’ Sredojevic amekitaja kikosi cha wachezaji 27 kuanza maandalizi muhimu kumenyana na Togo kufuzu katika fainali za kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi.

Mchuano huo utachezwa siku ya Alhamisi juma lijalo jijini Lome na kikosi hicho kinatarajiwa kuondoka jijini Kampala siku ya Jumatano kutumia ndege maalum iliyokodiwa na rais Yoweri Museveni.

Micho amesema ana imani na wachezaji aliowaita kambini.

Nina imani kubwa na hawa wachezaji niliyowaita kwa sababu wamekuwa wakifanya vizuri katika vlabu wanavyochezea.Tunataka kuwa na maandalizi mazuri kuelekea mchuano huo,” Micho ameimabia soka25east.com.

Mshambuliaji wa klabu ya Simba kutoka nchini Tanzania Hamis Kiiza ameitwa katika kikosi hicho pamoja na Ivan Bukenya anayecheza katika klabu ya Kaizer Chiefs nchini Afrika Kusini pamoja na Moses Oloya na Geofrey Baba Kizito.

Uganda na Togo watarudiana siku tatu baadaye jijini Kampala na mshindi atafuzu katika hatua ya makundi kutafuta tiketi ya kwenda Urusi mwaka 2018.

Kikosi kamili:

Makipa:

Denis Onyango, Salim Jamal, Robert Odongkara, James Alitho

Mabeki:

Dennis Iguma, Dennis Okot, Geofrey Walusimbi, Joseph Ochaya, Isaac Muleme, Shafiki Bakaki, Isaac Isinde, Ivan Bukenya, Murushid Jjuuko

Viungo wa Kati:

Tonny Mawejje, Aucho Khalid, Geofrey ‘Baba’ Kizito, Ivan Ntege, Yasser Mugerwa, Faruku Miya, William Luwaga Kizito, Muzamiru Mutyaba, Moses Oloya, Kezironi Kizito

Washambuliaji:

Geofrey Massa, Brian Umony, Hamis Kizza, Caesar Okhuti Ceaser

Must See

More in