Connect with us

Wagombea wa urais wa FIFA wafahamika

Wagombea wa urais wa FIFA wafahamika

Wagombea saba wanaotafuta urais wa Shirikisho la soka duniani FIFA wameanza kampeni kuomba kura kutoka mabara mbalimbali duniani.

Wanne kati ya wagombea hao wiki hii walizuru makao makuu ya mchezo wa soka barani Afrika CAF jijini Cairo nchini Misri kwenda kujitambulisha.

Bara la Afrika ambalo lina nchi 54 lina kura nyingi ukilinganisha na mabara sita ya FIFA na historia, inaonesha kuwa mshindi wa urais wa FIFA ni lazima aungwe kikamilifu na bara la Afrika.

Wagombea hao waliozuru Cairo ni pamoja na Sheikh Salman Bin Ibrahim Al-Khalifa rais wa Shirikisho la soka barani Asia, Mwanamfalme kutoka Jordan Ali Bin Al Hussein, Gianni Infantino Katibu Mkuu wa Shirikisho la soka barani Ulaya UEAFA na Tokyo Sexwale mfanyibiashara na mwanaharakati kutoka Afrika Kusini.

Orodha ya wagombea wote:

  • Prince Ali bin al-Hussein, miaka 39, rais wa Shirikisho la soka nchini Jordan
  • Musa Bility, miaka 48, rais wa Shirikisho la soka nchini Liberia.
  • Jerome Champagne, miaka 57, Mwanachama wa zamani wa Kamati kuu ya utendaji ya FIFA
  • Gianni Infantino, 45, Katibu Mkuu wa Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA
  • Michel Platini, miaka 60, rais wa Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA na Makamu wa rais wa FIFA
  • Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa, miaka 49, rais wa Shirikisho la soka barani Asia
  • Tokyo Sexwale, miaka 62, mwanasiasa, mwanaharakati na mfanyibiashara kutoka Afrika Kusini.

Uchaguzi huo umeratibiwa kufanyika mwezi Februari mwaka 2016.

Must See

More in