Connect with us

Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kesho wanaingia kwenye mchezo wa Kombe la FA bila kuwa na wachezaji wake kadhaa muhimu kutokana na sababu mbalimbali. Yanga kesho Jumapili itachuana na Reha FC kwenye Uwanja wa Uhuru, siku moja baada ya Simba kuvuliwa taji la Shirikisho kwa kufungwa na Timu ya

Wachezaji hao ni Donald Ngoma, Thabana Kamusoko, Pato Ngonyani na Kelvin yondani.

Donald Ngoma bado hajapona majeraha ya mguu  yanayomkabili wakati beki Kelvin Yondan anasumbuliwa na maumivu ya kifundo cha mguu na atakuwa nje kwa muda wa siku kumi hadi wiki mbili.

Kiungo Thaba Kamusoko bado hajaanza mazoezi na kikosi cha kwanza kutokana na kuwa nje kwa muda mrefu akikabiliwa na majeraha.

Kocha Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa amesema mcheoz huo ni muhimu kutokana na mipango ya timu hiyo kushinda vikombe vya Ligi ya ndani msimu huu.

“Ni mechi muhimu kwetu, wachezaji waliofanya mazoezi wako tayari kwa mchezo huo na matumaini yetu ni kushinda na kusonga mbele,”amesema Nsajigwa.

African journalist with passion of football reporting.Also i love politics

More in African Football