Connect with us

Yanga wakubali kumuacha Juma Balinya

Yanga wakubali kumuacha Juma Balinya

 YANGA WAKUBALI KUMUACHA JUMA BALINYA

Na Mwandishi wetu akiwa Dar Es Salaam,

Uongozi wa Yanga  SC kupitia kitengo cha idara ya habari na mawasiliano wametoa taarifa ya uongozi wa klabu hiyo kuridhia Ombi la Juma Balinya.

Mshambuliaji Juma Balinya kutokea Uganda aliomba kuvunja mkataba na Yanga SC ili awe huru kwenda kuanza maisha sehemu nyingine, hiyo inadaiwa ni kutokana na Yanga kutolipa malimbikizo ya mishahra.

Msemaji wa Yanga SC Hassan Bumbuli ameweka wazi taarifa na kueleza kwa kina kiwa uongozi wa Yanga huko tayari kukaa mezani na mchezaji wowote atakayeomba baraka za kwenda kutafuta maisha sehenu nyingine.

“Yanga imefikia makubaliano na mchezaji wetu Juma Balinya kuvunja mkataba kwa makubaliano, tulifikia makubaliano hayo baada ya mchezaji wetu Juma Balinya kuleta barua ya ombi hilo kwa sababu ya madeni yake ya mshahara wa miezi miwili na sisi tukaona tuna madai yetu ya msingi kimkataba hivyo tukaona tuachane nae” alisema Bumbuli

Must See

More in